• Skip to primary navigation
  • Skip to main content
  • Skip to primary sidebar
  • Skip to footer
ClickPesa

ClickPesa

Media

  • How does it work
  • Pricing
  • Solutions
    • e-Invoice
    • In-Store / Web Payments
    • Bulk Payments
  • Free Tools
    • Currency Converter
    • Income Tax PAYE Calculator
  • Knowledge Base
  • Login / Sign Up
Login

Namna ya kutangaza tovuti yako ya biashara mtandaoni.

October 6, 2021 by justine

Baada ya kutengeneza tovuti yako ya biashara mtandaoni, hatua inayofuata ni kuhakikisha kuwa unaitangaza ili kuwafikia watu wengi. Hatua ya 2 ya biashara kukua ni usambazaji. 

Kutokana na Tovuti za kihakiki kama google na facebook, 89% ya watumiaji watafanya manunuzi ndani ya wiki moja ya usomaji wa tahakiki hizo. Ndio maana unatakiwa kuitangaza tovuti yako ili kupata matokeo mazuri zaidi. 

Njia 7 za wazi za kutangaza Biashara yako Mtandaoni. 

Ujumbe kwa Video.

Linapokuaja suala la ujumbe mjongeo katika matangazo, video zinachukua nafasi ya kwanza. Video huwafikia watu wengi zaidi kuliko jumbe za kawaida na picha. Pia, video hutoa kiwango kikubwa cha taarifa katika muda mfupi. 

Tengeneza video zenye ubora wa hali ya juu kuhusu tovuti yako na kisha zisambaze katika majukwaa mbalimbali ili kuishirikisha hadhira yako. Unaweza kutengeneza video za kimatangazo na za kielimu. 

Kazi za Instagram 

Biashara katika Instagram zina shirikisha watu wengi mara 10 zaidi ya  Facebook, mara 54 zaidi ya  Pinterest na mara 84 zaidi kuliko Twitter.  Ingawa Instagram ilianza kama akaunti ya kutumia picha tu, kwa sasa imekua na kuwa jukwaa lenye nguvu kwa matangazo ya biashara za mtandaoni. 

Instagram inaweza kufaa zaidi kama unaihuisha biashara yako kwa kuonesha video za nyuma ya pazia kuhusu bidhaa na uzinduzi wa bidhaa zako. Hakikisha una “posti” tena posti za wateja wako kwa kutumia mtindo wa “hashitagi”.

Tumia Wahamasishaji

Linapokuja suala la kutumia wahamasishaji, ni lazima ujue ni jukwaa lipi la mtandao wa kijamii ni bora zaidi kwa ajili ya biashara yako. 

  • Teua wahamasishaji unaoweza kuwatumia; Hususani wahamasishaji wadogo wadogo.
  • Wape sampuli wahamasishaji wako ili watangaze bidhaa wanayoijua. 
  • Isome idadi na aina ya wafuasi katika akaunti yako na ujue ni vitu gani huwafanya wawe macho navyo.  

Jenga Jamii kwa kutumia blogu yako.  

Watu katika mtandao wataanza kujenga imani ikiwa wanakuona wewe kama mtaalamu katika kampuni  yako. Njia bora ya kujenga uaminifu ni kutoa maudhui yenye thamani na ya kuaminika katika blogu yako. Wanaweza kutumia taarifa hizi kufanya maamuzi sahihi. 

Pia unaweza kuandika makala kuhusu makampuni yanayohusiana na kampuni yako lakini si makampuni shindani katika biashara yako. Kwa mfano, kama unauza fremu za picha za ukutani, kuwa karibu na tovuti zinazohusu mitindo ya ndani ya nyumba. 

Kujihusisha na Tovuti Maarufu za Mijadala. 

Mbinu moja kubwa ya kusambaza biashara yako ya mtandaoni ni kwa kujichanganya na mijadala maarufu katika tovuti zenye  idadi kubwa ya watazamaji. Majukwaa ya kijamii kama Africaweb (yenye watazamaji 98m+) na Reddit ambayo imeshika nafasi ya 18 katika dunia nzima kwa kuwa na watazamaji wengi inaweza kuwa chaguo zuri zaidi. 

Unatakiwa uweke mjadala wako katika sehemu ambayo kiungo cha tovuti yako kinaweza kuonwa na hivyo kutazamwa na watu wengi. Majukwaa mengine kama Clubhouse, Facebook, na Jamiiforums yanaweza kukusaidia kutaja akaunti yako katika mjadala njia ambayo itasaidia watu kukutafuta kwa matarajio ya haraka. 

Familia na Marafiki

Wafikie wanafamilia na marafiki zako kwa kuwajulisha kuhusu tovuti yako na inatoa huduma gani. Mapendekezo ya watu binafsi binafsi huaminika kwa kiasi kikubwa sana. Marafiki zako na wanafamilia wanaweza kupendekeza biashara yako ya mtandaoni kuiingiza katika mitandao yao. Hii imekuwa ni mbinu kubwa inayotumiwa na makampuni ya MLM kwa miongo mingi.

Usiwe unakosa kwenye matukio mbalimbali ya hadhara. Matukio ya hadhara yanaweza kukupa nafasi ya kukutana na hadhira kubwa kwa muda mfupi. 

Kwa kuhitimisha, majukwaa kama clickpesa.com yana mambo ya msingi na msaada unaoweza kupima duka la biashara yako ya mtandaoni. Uwe unatangaza biashara yako mtandaoni au nje ya mtandao, unapaswa kuwa mbunifu na kuwa tayari kuwageuza wateja watarajiwa wako na mwisho kuwa wateja. 

Category iconUncategorized

Primary Sidebar

Open an account for your organization

Create your ClickPesa account, connect your bank or mobile money account within seconds. Start to receive and make payments.

Recent Articles

7 Reasons Why You Need Payment Automation For Your Business Growth.

October 20, 2022

What is payment automation? Businesses can make … [Read More...] about 7 Reasons Why You Need Payment Automation For Your Business Growth.

5 Reasons Companies Should Accept Multiple Payment Methods in Kenya

September 10, 2022

With the digital economy evolving rapidly, … [Read More...] about 5 Reasons Companies Should Accept Multiple Payment Methods in Kenya

Benefits of electronic invoicing.

July 29, 2022

Electronic invoicing, which is also known as … [Read More...] about Benefits of electronic invoicing.

The future of digital payments

June 6, 2022

The 21st century gift of the internet has … [Read More...] about The future of digital payments

Create your account


Login / Sign Up



Subscribe to receive our latest updates


Footer

Legal

  • Terms and Conditions
  • Privacy Policy
  • Data Retention Policy

Company

  • About Us
  • Our Leadership
  • Contact Us
  • Jobs
  • Insights
  • Investors

Learn

  • Bizfundi
  • Entrepreneur by TPSF
  • BRELA

Solutions

  • e-Invoice
  • In-Store / Online Payments
  • Bulk Payments
  • Payout Services

Community

  • Facebook
  • Instagram
  • LinkedIn
  • Medium
  • Twitter
  • YouTube

Address

Tanzania Office
Victoria Place, Kibisho Street, 102, Dar es Salaam

UK Office
71-75 Shelton Street, London, Greater London, United Kingdom, WC2H 9JQ

clickpesa-logo-vertical

ClickPesa works with licensed financial institutions governed by central banks across the globe. Funds in transaction are securely held at all times by licensed financial custodians with deposit guarantees. Read More




© ClickPesa Limited – All Rights Reserved

By using this website, you agree to our use of cookies. We use cookies to provide you with a great experience and to help our website run effectively.OkPrivacy policy