Baada ya kutengeneza tovuti yako ya biashara mtandaoni, hatua inayofuata ni kuhakikisha kuwa unaitangaza ili kuwafikia watu wengi. Hatua ya 2 ya biashara kukua ni usambazaji.
Kutokana na Tovuti za kihakiki kama google na facebook, 89% ya watumiaji watafanya manunuzi ndani ya wiki moja ya usomaji wa tahakiki hizo. Ndio maana unatakiwa kuitangaza tovuti yako ili kupata matokeo mazuri zaidi.
Njia 7 za wazi za kutangaza Biashara yako Mtandaoni.
Ujumbe kwa Video.
Linapokuaja suala la ujumbe mjongeo katika matangazo, video zinachukua nafasi ya kwanza. Video huwafikia watu wengi zaidi kuliko jumbe za kawaida na picha. Pia, video hutoa kiwango kikubwa cha taarifa katika muda mfupi.
Tengeneza video zenye ubora wa hali ya juu kuhusu tovuti yako na kisha zisambaze katika majukwaa mbalimbali ili kuishirikisha hadhira yako. Unaweza kutengeneza video za kimatangazo na za kielimu.
Kazi za Instagram
Biashara katika Instagram zina shirikisha watu wengi mara 10 zaidi ya Facebook, mara 54 zaidi ya Pinterest na mara 84 zaidi kuliko Twitter. Ingawa Instagram ilianza kama akaunti ya kutumia picha tu, kwa sasa imekua na kuwa jukwaa lenye nguvu kwa matangazo ya biashara za mtandaoni.
Instagram inaweza kufaa zaidi kama unaihuisha biashara yako kwa kuonesha video za nyuma ya pazia kuhusu bidhaa na uzinduzi wa bidhaa zako. Hakikisha una “posti” tena posti za wateja wako kwa kutumia mtindo wa “hashitagi”.
Tumia Wahamasishaji
Linapokuja suala la kutumia wahamasishaji, ni lazima ujue ni jukwaa lipi la mtandao wa kijamii ni bora zaidi kwa ajili ya biashara yako.
- Teua wahamasishaji unaoweza kuwatumia; Hususani wahamasishaji wadogo wadogo.
- Wape sampuli wahamasishaji wako ili watangaze bidhaa wanayoijua.
- Isome idadi na aina ya wafuasi katika akaunti yako na ujue ni vitu gani huwafanya wawe macho navyo.
Jenga Jamii kwa kutumia blogu yako.
Watu katika mtandao wataanza kujenga imani ikiwa wanakuona wewe kama mtaalamu katika kampuni yako. Njia bora ya kujenga uaminifu ni kutoa maudhui yenye thamani na ya kuaminika katika blogu yako. Wanaweza kutumia taarifa hizi kufanya maamuzi sahihi.
Pia unaweza kuandika makala kuhusu makampuni yanayohusiana na kampuni yako lakini si makampuni shindani katika biashara yako. Kwa mfano, kama unauza fremu za picha za ukutani, kuwa karibu na tovuti zinazohusu mitindo ya ndani ya nyumba.
Kujihusisha na Tovuti Maarufu za Mijadala.
Mbinu moja kubwa ya kusambaza biashara yako ya mtandaoni ni kwa kujichanganya na mijadala maarufu katika tovuti zenye idadi kubwa ya watazamaji. Majukwaa ya kijamii kama Africaweb (yenye watazamaji 98m+) na Reddit ambayo imeshika nafasi ya 18 katika dunia nzima kwa kuwa na watazamaji wengi inaweza kuwa chaguo zuri zaidi.
Unatakiwa uweke mjadala wako katika sehemu ambayo kiungo cha tovuti yako kinaweza kuonwa na hivyo kutazamwa na watu wengi. Majukwaa mengine kama Clubhouse, Facebook, na Jamiiforums yanaweza kukusaidia kutaja akaunti yako katika mjadala njia ambayo itasaidia watu kukutafuta kwa matarajio ya haraka.
Familia na Marafiki
Wafikie wanafamilia na marafiki zako kwa kuwajulisha kuhusu tovuti yako na inatoa huduma gani. Mapendekezo ya watu binafsi binafsi huaminika kwa kiasi kikubwa sana. Marafiki zako na wanafamilia wanaweza kupendekeza biashara yako ya mtandaoni kuiingiza katika mitandao yao. Hii imekuwa ni mbinu kubwa inayotumiwa na makampuni ya MLM kwa miongo mingi.
Usiwe unakosa kwenye matukio mbalimbali ya hadhara. Matukio ya hadhara yanaweza kukupa nafasi ya kukutana na hadhira kubwa kwa muda mfupi.
Kwa kuhitimisha, majukwaa kama ClickPesa yana mambo ya msingi na msaada unaoweza kupima duka la biashara yako ya mtandaoni. Uwe unatangaza biashara yako mtandaoni au nje ya mtandao, unapaswa kuwa mbunifu na kuwa tayari kuwageuza wateja watarajiwa wako na mwisho kuwa wateja.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.